Tovuti hii imeanzishwa na Benson Mahenya ili kutoa jukwaa la kupashana
habari na kuelimishana miongoni mwa wanamtandao si wa hapa Tanzania tu bali duniani kote.
Kwa kuanzia tutatumia lugha za Kiswahili na Kiingereza. Siku za usoni tutaongeza lugha
nyingine kama Kifaransa, Kichina, Kitaliano, Kispaniola, Kireno, Kihindi n.k.
|
|
Benson Mahenya ni mwanamtandao mahiri
ambaye kwa miaka takribani miwili amekuwa akifanya biashara ya mtandao na
kampuni moja ya kimataifa inayofanya kazi katika nchi zipatazo 140 na ambayo
mauzo yake ya mwaka yapata USD2.5 billion. Baada ya kusoma machapisho mbali
mbali na kufundisha watu mikoa mbali mbali nchini Tanzania na nchi za Afrika Mashariki
na kusini mwa Afrika kuhusu biashara ya mtandao amegundua ukosefu mkubwa wa vitabu
vya Kiswahili kwa wazungumzaji wa lugha ya Kiswahili. Hata wale wanaojua kiingereza
hawafanyi jitihada za makusudi za kusoma na kujiendeleza katika fani hii. Ni imani yake
kuwa tovuti hiki itawasaidia wasomaji wa lugha ya Kiswahili Afrika Mashariki na duniani
kote kuweza kuelewa nini maana ya biashara ya mtandao. Benson anakusudia kufanya
kazi kwa karibu na vitivo vya biashara na idara za masoko za vyuo vyote vya elimu ya
juu hapa Tanzania, Afrika Mashariki na kwingineko ili kuhakikisha biashara ya mtanda
o inapata nafasi stahili katika mitaala ya kozi za masoko na ujasiriamali.
Benson alihitimu katika Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam na kutunukiwa shahada daraja la kwanza katika
masuala ya fedha na uongozi (BCom). Benson alishinda skolaship ya Jumuiya
ya Madola iliyomuwezesha kwenda Uskochi (Scotland) ambako alisomea shahada ya
pili ya masuala ya fedha (MSc) kabla ya kuhitimu tena katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
katika masuala ya masoko (MBA). Benson pia ni mhitimu wa cheti cha juu cha uhasibu (CPA)
na amewahi kufanya kazi katika mashirika mbali mbali ya kimataifa katika sekta ya benki na
ukaguzi wa mahesabu kabla ya kuanzisha shughuli zake binafsi za ushauri wa kibiashara na
ukaguzi. Benson amesafiri nchi nyingi duniani na anapenda kuwasaidia wajasiriamali wachanga
katika biashara zao.
Benson ni mume wa Susan na wana watoto wawili Tusekelege
na Gwamaka ambao tayari wanaelewa vilivyo,
katika umri wao mdogo, nini biashara ya mtandao!
|
Facts on Zanzibar
The island is located in the Indian ocean about 35 Km of the coast of mainland Tanzania at six degrees south of equator. Zanzibar is made up of many islands, the main two being Unguja...
Click here for more |
Bagamoyo
Bagamoyo is located almost 65 km from the city Centre,Bagamoyo is the
most atractive place,our buses will take you
there under agreed arangement
Click here for more
|
Serengeti National park
The Serengeti region encompasses the Serengeti National
Park itself, the Ngorongoro Conservation Area,
Click here for more
|
Ngorongoro Crater
The Ngorongoro Conservation Area or NCA is a conservation area situated 180 km west of Arusha in the Crater Highlands area of Tanzania. The conservation area's boundaries follow the
Ngorongoro District. It is 8,288 km˛
Click here for more |
Bagamoyo
Bagamoyo is located almost 65 km from the city Centre,Bagamoyo is the
most atractive place,our buses will take you
there under agreed arangement
Click here for more
|
Serengeti National park
The Serengeti region encompasses the Serengeti National
Park itself, the Ngorongoro Conservation Area,
Click here for more
|
Welcome to Network Marketing Tanzania- - All rights reserved P.O. Box , Dar Es Salaam , Tanzania -
Mob: +255 716 954 840- Fax: +255 22 2461 066 Email: info@networkmarketingtz.com - Design by Sam Mujinja E-mail mujinja@hotmail.com Mob: +255 713 451713,
|
|